Alhamisi , 28th Apr , 2022

Serikali imepanga kuongeza bajeti Kwa asilimia 11 kwa shirika la umeme nchini TANESCO Ili kuhakikisha linafanya maboresho katika Miundombinu yake.

Hayo yemesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Maharage Chande katika kipindi maalum Cha TANESCO na wadau wakijumuishwa waandishi wa habari akibainisha kuwa shirika linakwenda kupambana na uchakavu wa mitambo unaosababisha kukatika kwa umeme Mara kadhaa na kuleta adha kubwa Kwa wananchi.

"Lengo la serikali kuongeza bajeti hii ni kutaka kuona matokeo na ubora wa Huduma hii ikihisisha bajeti ya matengenezo"alisema Maharage.

Sambamba na hilo amesema shirika sasa limezindua mifumo ya kisasa ambapo mteja ataweza kujaza fomu kuwasilisha Tatizo lake kupitia njia ya mtandao ambayo imetajwa kuwa rafiki yenye kuepusha vitendo vya rushwa.

"Huu mfumo unaitwa Niconnet ambapo mteja atajaza fomu huko huko aliko na mafundi watamfikia hii yote tumelenga kufanya kazi kisasa kulingana na teknolojia"alisisitiza Maharage.

EATV imeenda mbali zaidi na kuzungumza na wachumi akiwemo Walter Nguma ambaye amesema Kwa kipindi kirefu taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali zimeoneesha ubadhilifu katika Miradi mingi ya mashirika ya kiserikali hivyo Wana Imani kuwa mfumo wa Niconnet unaweza kudhibiti ubadhilifu uliokuwa ukifanyika.

"Watanzania wanatamani kuona Tanesco ikifanya mabadiliko Kwa kuwa Nishati ndiyo Kila kitu na tukiitumia Teknolojia vyema tunaamini matunda yataonekana"alisema Walter.

Kuhusu ujenzi mkubwa wa mradi bwawa la mwalimu Nyerere unaoendelea Maharage Chande amesema Hadi sasa umefika asilimia 58.