Ijumaa , 26th Sep , 2014

Serikali ya Tanzania imesema kuwa imejipanga vizuri katika kuilinda nchi kutokana na vitisho na matukio ya ugaidi yanazozikabili nchi za Afrika Mashariki hususani nchi jirani ya Kenya.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Bernad Membe

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania Bernad Membe katika mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa kwenye Kikao cha pembeni cha nchi za SADC.

Membe amesema kuwa Watanzania hawatakiwi kuwa na wasiwasi kuhusiana na matukio ya ugaidi kushambulia Tanzania kwa kuwa vyombo vya usalama nchini vimejipanga vyema kuweza kukabiliana na hali hiyo.