Jumamosi , 9th Apr , 2016

Makamu wa Rais nchini Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan amesema kuwa serikali iko tayari kuwapokea wawekezaji ambao wakotayari kufuata masharti ya uwekezaji nchini ikiwa pamoja na kulipa kodi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Palm Village katika eneo la Msasani, mradi unaofanywa na kampuni ya kichina ya Group Six ambapo Mhe. Suluhu ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha kuwa inafuata taratibu zote za uwekezaji ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Aidha makamu wa Rais amesema ujenzi wa nyumba hizo utaongeza upatikanaji wa shughuli za kijamii na kuinua uchumi sambamba na kuongeza idadi ya mali zisizohamishika nchini ambapo Mhe. Suluhu ameisisitiza kampuni hiyo kuhakikisha kuwa kazi zinazoweza kufanywa na watanzania waachiwe watanzania wenyewe.