Jumatano , 27th Apr , 2022

Kwa mujibu wa tovuti ya Business Inside Africa, Tanzania inashika nafasi ya pili katika orodha ya nchi 7 zilizopata watalii wengi wa nje kwa mwaka 2021 barani Afrika.

Tanzania ilipata watalii wa nje 900,000 kwa mwaka 2021.

Tanzania inashika nafasi ya pili kwa idadi ya watalii laki 9, nyuma ya Afrika Kusini iliyokuwa na watalii millioni 2.3 kwa mwaka 2021.

1. Afrika Kusini - 2,300,000
2. Tanzania - 900,000
3. Ethiopia - 500,000
4. Reunion - 300,000
5. Eswatini - 200,000
6. Visiwa vya Shelisheli - 200,000
7. Mauritius - 200,000