Jumatano , 30th Sep , 2015

Tanzania imekua nchi ya pili barani Afrika kuwa na chuo cha kijeshi cha sayansi za tiba chenye ukubwa na vifaa vya kisasa vya kutolea mafunzo ya sayansi za tiba ngazi ya shahada kwa wanajeshi wa hapa nchini na wale wanaotoka nchi mbalimbali za SADC

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Dkt. Hussein Mwinyi.

Uwepo wa chuo hicho cha kijeshi cha sayansi za tiba kilichozinduliwa jijini Dar es Salaam jana kumefanikishwa na serikali ya Ujerumani kwa kutoa msaada wa zaidi ya Euro miloni 3 kwa serikali ya Tanzania.

Akizungumza katika uzunduzi huo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amesema chuo hicho kitaweza kutoa nafasi kwa wanajeshi nchini Kujifunza zaidi lakini pia kutoa nafasi ya nchi nyingine kujiunga kwa lengo la kupata mafunzo.

Kwa upande wake balozi wa Ujerumani nchini Tanzania bw. Egon Konchake amesema nchi hiyo imefikia hatua ya kutoa msaada huo kutokana na mahusiano ya ukaribu katika maendeleo baina ya nchi hizo.