
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge.
Waziri wa nchi, ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt. Binilith Mahenge ametoa taarifa ya kuwepo kwa mkutano huo ambao moja ya ajenda zake ni kujadili mkakati wa pamoja wa kuzitaka nchi zilizoendelea kiviwanda, ziwajibike na kuifidia Afrika kutokana na kuhusika na uharibu wa mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa Waziri Mahenge, nchi za Afrika zina wajibu wa kutaka nchi zilizoendelea kiviwanda ikiwemo Marekani na mataifa ya Ulaya, ziwajibike kutokana nchi hizo kutoa zaidi ya asilimia tisini na saba ya gesi ukaa ambayo ni hatari kwa mazingira, wakati bara la Afrika likitoa asilimia tatu tu lakini ndio linaloathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa waziri Mahenge, umuhimu wa nchi za Afrika kufidiwa inatokana na ukweli kwamba nchi hizo hazina uwezo wa kukakibiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi kama vile ukame, mafuriko na magonjwa ya milipuko.