Jumapili , 4th Dec , 2022

Kutokana na Ofisi ya Tawi la Mtakuja  la Chama Cha Mapinduzi CCM katika kata ya Kunduchi kufanya vikao katika miti Tawi hilo limepokea msaada wa matofali 200 kutoka kwa mdau wa maendeleo na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo.

Akizungumza na EATV jijini Dar es salaam Katibu wa Tawi hilo Sharifa Kitenge amesema wameshukuru kupokea tofali hizo kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta mfadhili kwa ajili ya kupata mdhamini kwa ajili ya ujenzi wa Tawi hilo.

Aidha amesema kuwa matofali hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katjika ukarabati wa ofisi hiyo ambayo bado inahitaji mamboresho makubwa kwani bado wanafanya vikao katika sehemu zisizo rasmi.

Kwa upande wake mdau  wa maendeleo na Mwanachma wa Chama Cha Mapinduzi Omary Hassan amesema amekabidhi tofali hizo mara baada ya kuona uhitaji wa tofali kwani jengo hilo ni la muda mrefu na limechakaa.

Pia ameongeza kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa vya ujenzi ili ofisi hiyo ikamilike na iwe katika hali nzuri hivyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza.