Jumatano , 20th Jul , 2016

Kaimu mkurugenzi wa shirika la viwango nchini Tanzania TBS Dkt.Egid Mubofu amekemea wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanatumia njia za panya kuingiza bidhaa zilizo chini ya kiwango nchini.

Kaimu mkurugenzi wa shirika la viwango nchini Tanzania TBS Dkt.Egid Mubofu amekemea wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanatumia njia za panya kuingiza bidhaa zilizo chini ya kiwango nchini.

Dkt.Mubofu ameyasema hayo katika mahojiano maalum na East Africa Television na kuongeza kuwa tayari wamewakamata baadhi ya wafanyabisahara ambao wamekuwa wakijihusisha na uingizwaji wa bidhaa ambazo zipo chini ya ubora wa kiwango.

Amesema katika kuhakikisha kwamba bidhaa zinazoingizwa nchini zinakuwa na ubora wa viwango vya kimataifa ni lazima jamii iwafichue wahusika wa uhalifu huo ili kuhakikisha taifa linaingia fedha nyingi za kigeni ambazo zitawezesha taifa kuingizwa katika ushindani wa soko la kimataifa.

Wanashirikiana na taasisi zingine katika kuhakikisha wanasimamia ubora wa bidhaa zinazoingizwa na kutengenezwa nchini ili kulinda afya ya mtumiaji.