
Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo na mamlaka hiyo, imesema kuwa Helikopta hiyo imepewa kibali cha muda mrefu (block permit) na TCAA kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kuanzia Septemba 4 hadi Oktoba 31, 2020 na kukanusha madai hayo.
Mkurugenzi Mkuu TCCA, Hamza Johari amekanusha pia uwepo wa ofisa wa mamlaka hiyo aliyetoa taarifa kuhusu safari ya msafara wa Mhe. Lissu kutokuwepo kwani safari ya CHADEMA haikuwepo kwenye orodha.
Ufafanuzi huo wa TCAA umekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene kuwa helikopta iliyokuwa itumike na Tundu Lissu ilizuiliwa na mamlaka hiyo.
Taarifa kamili ya TCAA hii hapa chini.