Ijumaa , 10th Feb , 2023

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limevipongeza vyombo vya habari kwa umoja katika kupambania muswada wa huduma wa vyombo vya habari kusomwa leo bungeni.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile, ameeleza hayo leo, huku akihimiza tamko waliolitoa halikulenga kumlaumu mtu, bali walikuwa wanapambania haki yao.

Aidha Jukwaa limeendelea kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kusimamia misingi ya uhuru wa vyombo vya habari nchini, jambo linalochochea upatikanaji wa taarifa kwa wananchi na kuwa msingi bora wa utawala bora.

TEF wameahidi kuendelea kupigania haki ya watu kupata taarifa, huku pia viongozi wengine wa TEF wakashukuru kwa muswada huo kusomwa bungeni leo. 

Februari 8, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) lilitoa tamko la  kusikitishwa na kauli ya Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kuwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari (MA 2016) umeshindikana kuingizwa bungeni kutokana na ripoti nyingi za Kamati za Kisekta za Bunge.