Alhamisi , 27th Oct , 2016

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeainisha maeneo ya ubunifu ndani ya sera mpya ya Teknlojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kufanikisha utatuzi wa masuala mbalimbali katika jamii na kuondoa changamoto ya ajira kwa vijana.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora

Pia ili kurahisisha mawasiliano na utendaji kazi wa serikali sambamba na kuboresha kilimo kupitia TEHAMA (Smart Agriculture).

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa tathmini ya mradi wa teknolojia ya mawasiliano kati ya Tanzania na nchi ya Finland TANZAICT, Katibu Mkuu wa Mawasiliano kutoka Wizara hiyo Prof. Faustine Kamuzora amesema Tanzania inalenga kufikia uchumi wa kati kupitia TEHAMA kwa kuhuisha shughuli za uzalishaji, makusanyo ya mapato, elimu na kupeleka huduma za jamii hususan za kiafya kupitia Tehama.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Larex Lishokeleza, amesema kwa sasa wanalenga kuangalia ubunifu unaofanywa na vijana katika kuongeza ubora wa matumizi ya TEHAMA katika kutatua changamoto mbalimbali.