Jumatatu , 28th Mar , 2016

Halmashauri za wilaya na Manispaa Mkoani Katavi zimetakiwa kusimamia miradi inayojengwa kwa gharama nafuu na ubora unaotakiwa huku wakitumia wakandarasi wenye uwezo kuleta thamani halisi ya miradi hiyo.

Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Katavi, William Mbogo,

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Katavi, William Mbogo,mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Nsimbo.

Mhe. Mbogo amesema kuwa Halmashauri nyingine nchini zinatakiwa kujifunza kutoka halmashauri ya Nsimbo, ambapo wamejenga majengo yenye ubora wa hali ya juu lakini yakiwa na gharama nafuu huku pia yakiwa yamekamilika kwa wakati.

Akizungumza Ujenzi wa Majengo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo, Michael Nzungu amesema kuwa tenda hiyo waliowakadhabidhi Suma Jkt, imeweza kukamilika kwa muda wa miezi sita ni kutokana na usimamizi mzuri kutoka kwao na ufanyanyi kazi bora wa Suma Jkt.

Nao baadhi ya Wajumbe wa Alat walizungumzia changamoto zinazowakabili katika halmashauri zao ni pamoja na tenda kugawiwa zikiwa na harufu za rushwa kitu ambacho kinarudisha maendeleo nyuma.