
Kauli hiyo ya halmashauri ya wilaya ya Temeke imetolewa na mwakilishi wa mkuu wa wilaya hiyo Bw. Sadati Mohammed alipomuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika uzinduzi wa maabara ya kompyuta katika shule ya sekondari Uhamiaji iliyopo katika halmashauri hiyo.
“tunashukuru sana kwa niaba ya wilaya kwa maono haya ya kuanzisha maabara ya komputa, sasa wanafunzi wataweza kujifunza kwa vitendo maana awali walikuwa wanajufunza kwa nadharia. Sasa tutalifikisha ngazi za juu lakini kabla hawajatuletea hao waalimu, sisi manispaa ya Temeke tutaleta walimu wa muda na tutawalipa ili waweze kutufundishia watoto somo hili la Kompyuta” - Sadati Mohammed, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Temeke.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maabara hiyo, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhamiaji amesema kuwa uwepo wa maabara hiyo utawasaidia wanafunza kuelewa wanachojifunza hukuku mmoja wa wanafunzi akieleza kuwa kama wanafunzi kompyuta hizo zitawasaidia kupata maandiko mbalimbali ya masomo tofauti wanayosoma shuleni hapo.
“uwepo wa maabara hii tatusaidia sisi walimu kuwafundisha watoto, lakini pia italeta chachu kwa wanafunzi kupenda na kuwa na ujuzi wa kiteknolojia na ubunifu. Hapo awali hatuluwa na maabara kwahiyo mtoto anafundishwa lakini hata Komputa yenyewe haijui inawashwa vipi, kwahiyo hii itasaidia sana kujua vifaa vya kielektroniki” - Mwl. Boaz Ndyakalika, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhamiaji.