
Trump amesema hayo wakati wa hotuba mbele ya maelfu ya waombolezaji katika ibada ya kumbukumbu huko Arizona kufuatia kuuawa kwake
Trump alikuwa mzungumzaji mkuu katika hafla hiyo iliyojaa watu Jumapili, ambapo maafisa wakuu kutoka kwa utawala wake, akiwemo Makamu wa Rais JD Vance, walisifu urithi wa kisiasa wa Kirk baada ya kupigwa risasi tarehe 10 Septemba.
Amesema aliuawa kwa sababu aliishi kwa ujasiri, na alibishana kwa ustadi,
Mke wa Kirk, Erika, pia alitoa hotuba ya maombolezo iliyojawa simanzi alisema alimsamehe anayedaiwa kuwa muuaji wa mumewe.
Maelfu ya watu walipanga foleni kwa saa nyingi nje ya uwanja kabla ya tukio hilo, huku wengine wakipiga kambi usiku wa kuamkia jana ili kupata nafasi ya kumuomboleza.