Jumatano , 30th Apr , 2014

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania TUCTA, limesema hali ya wafanyakazi nchini ni mbaya kwani wengi wao wanaishi maisha ya huzuni na kusononeka.

Katibu mkuu wa TUCTA, Nicholas Mgaya

Katibu Mkuu wa TUCTA Bw. Nicolas Mgaya amesema hayo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tu kabla ya wafanyakazi nchini hawajaungana na wafanyakazi wengine Duniani kusherehekea siku ya wafanyakazi Mei Mosi hapo kesho.

Bw. Mgaya amesema sababu zinazochangia kusononeka wafanyakazi ni pamoja na kutokuwa na uhakika wa maisha kutokana na kulipwa mishara duni ambayo hata hivyo huandamana na mlolongo wakodi alizoziita kuwa ni kandamizi.