
Katibu mkuu wa TUCTA, Nicholaus Mgaya
Aidha wamesema kilio hicho kitawasilishwa kwa serikali katika Sikukuu ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi mwaka huu na kwamba kero ambazo bado zinawakabili wafanyakazi nchini ni Mishahara duni, kodi kubwa na kiwango kidogo cha Pensheni.
Akizungumza jijini Dar-es-salaam Katibu Mkuu wa TUCTA Nicholas Mgaya alisema sherehe hizo kitaifa zitafanyika jijini Dar-es-salaam na Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uwanja wa Uhuru.