Jumamosi , 15th Oct , 2016

Waziri wa Ardhi Nyumba na Manendeleo ya Kazi Willium Lukuvi amezindua Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi nchini, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa ardhi Willium Lukuvi alipokuwa akizindua Kamisheni ya Tume ya Matumizi ya Ardhi Jijini Dar ers salaam.

Akizungumza wakati wa tukio hilo Waziri Lukuvi ameiongezi kwa kamisheni hiyo huku akiamini uwajibikaji wao kwamba utasaidia sana sekta ya ardhi nchini kufanya vyema.

“Napenda nitumie fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwako wewe Mwenyekiti pamoja na Makamishna Wateule wote wa Bodi ya Tume yaTaifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kuteuliwa kwenu kuwawasimamizi wa shughuli za Tume hii. Nimepata taarifa kwamba, pamoja nauzinduzi wa Bodi hii kufanyika leo, tayari mlishaanza utekelezaji wamajukumu yenu” Amesema Lukuvi

Lukuvi ameongeza kuwa Sheria ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya Mwaka 2007, imetungwakutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kuratibu na kusimamiaupangaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.Utekelezaji wa jukumu hili unahusisha taaluma za sekta anuai kwa azma yakutumia vizuri rasilimali zote za ardhi ili kuleta maendeleo endelevu nakuondoa umaskini.

Aidha Sheria ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya Mwaka 2007, imetungwakutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kuratibu na kusimamiaupangaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.Utekelezaji wa jukumu hili unahusisha taaluma za sekta anuai kwa azma yakutumia vizuri rasilimali zote za ardhi ili kuleta maendeleo endelevu nakuondoa umaskini.

Pamoja na hayo Waziri Lukuvi amesema serikali itaisaidia tume hiyo kukabiliana na changamoto zinazoikabili ili iweze kutimiza majukumu yake yaliyoainishwa kisheria.

Kuundwa kwa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ni hatuamuhimu sana kwa nchi yetu katika matumizi endelevu ya rasilimali za ardhi nchini.