Jumatatu , 19th Nov , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amebainisha kuwa Mkoa wake unatarajiwa kupanua moja ya gereza mkoani humo ili kuhakikisha wanawasweka ndani watu ambao amewadai kupindisha kile ambacho amekuwa akikiagiza kifanyike.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Akizungumza katika kongamano lililolenga kuhamasisha kuelekea ujenzi wa mradi wa Umeme wa Stiglers George ambao unatajwa huenda ukamaliza uhaba wa Umeme nchini.

Akiwa kwenye kongamano hilo lililohudhuriwa na Waziri wa Nishati, Merdadi Kalemani, Chalamila amesema “Mbarali tangu 2008 migogoro haimaliziki, sasa hivi nina mpango wa kutanua magereza kwa ajili ya kuwasweka ndani wasiosikia, nchi hii  tusiicheleweshe makusudi.”

Pale Mbeya kuna watu walitaka kubembelezwa kulipa kodi, kuna mambo watu watatii sheria kwa shuruti, kwa hiyo kuna mahali taifa lilikuwa na watu wasanii,” ameongeza Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila.

Katika kongamano hilo wadau mbalimbali kutoka mikoa ambayo inaunganishwa na mradi huo wa Stiglers George walitoa maoni yao pamoja na kufahamishwa fursa zitakazopatikana kwenye mradi huo.