
Mgombea urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu.
Akizungumza katika mkutano wake wa kampeni mkoani Geita katika kata ya Nkome, Lissu, ameahidi tume hiyo itachunguza matukio ya ukiukwaji haki za binadamu katika maeneo yote ya uvuvi nchini.
"Tutakapounda serikali nikiwa rais wenu, tutaunda tume ya uchunguzi ya majaji itakayochunguza matukio yote ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo yote ya uvuvi”, amesema Lissu
Aidha Lissu amesema kuwa serikali yake endapo itaingia madarakani itahakikisha wananchi wanavua samaki bila kubugudhiwa, "Tunataka wananchi wa Nkome na wananchi wa maziwa yote ya Tanzania iwe Tanganyika, Victoria, Nyasa na maziwa mengine madogomadogo pamoja na ukanda wa Bahari ya Hindi, waweze kuvua samaki kulisha familia zao na kutulisha sisi wengine tusiokuwa wavuvi bila kubugudhiwa".