Alhamisi , 5th Jun , 2014

Zaidi ya watoto 150 wenye umri chini ya miaka mitano wamepoteza  maisha tangu mwaka jana hadi sasa kutokana na kukosa miundombinu ya barabara wilayani Nkasi mkoani Rukwa

Baadhi ya wakazi wa Nkasi wakiwa katika usafiri wa mtumbwi kuelekea katika kituo cha afya

Zaidi ya watoto 150 wenye umri chini ya miaka mitano wamepoteza  maisha tangu mwaka jana hadi sasa kutokana na kukosa miundombinu ya barabara na usafiri wa njia ya maji usio wa uhakika kutoka katika visiwa vya kata za kipili, ninde na kirando kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Kaimu mganga mkuu wilaya ya nkasi DK. Makundi Mazige ameyasema hayo katika taarifa yake ya mradi wa uhamasishaji wa ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia, amesema wananchi wa vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika kwa kukosa barabara na kutegemea mitumbwi hujikuta wanapeleka wagonjwa hospitali wakiwa katika hali mbaya ya kuchelewa na wakati mwingine wakiwa wameisha fariki.

Kwa upande wake diwani wa kata ya kiili Basilio Kapunda amesema wananchi wanaotegemea usafiri wa mitumbwi wanafikia takribani theluthi mbili ya wakazi wa wilaya nzima ya Nkasi, na kusema kuwa usafiri huo wa mitumbwi ya kienyeji ni hatari na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi kutokana na hali ya hewa kuchafuka mara kwa mara.

Pia ameeleza kuwepo changamoto ya kituo cha afya cha kirando kufanya kazi nje ya uwezo wake ikiwemo kupokea wagonjwa kutoka nchi ya jirani ya kongo kupitia njia ya ziwa hilohilo:

Akizungumzia kadhia hiyo mkurugenzi wa halmashauri ya Nkasi bw. Kimulika Galikunga pamoja na kukiri uduni wa miundombinu ya barabara katika hamlashauri hiyo hususan vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika, amesema katika kipindi cha mwaka huu wa fedha watatengeneza sehemu ya barabara hizo, huku akieleza kupitia mradi wa mama na mwana kuweka maboti mawili ya huduma za wagonjwa katika ziwa Tanganyika kama mpango wa dharura huku wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu: