
Tangazo hilo lililotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibatr imebainisha kuwa wagombea wote walioteuliwa hapo awali ndio watakao kuwa wagombea katika uchaguzi huo.
Vile vile Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni.
Aidha Chama cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikipinga kurudiwa kwa uchaguzi. Chama hicho mapema mwezi huu kilionya kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha vurugu, huku Chama cha Mapinduzi kikiwataka wanachama wake kujipanga kwa uchaguzi.
Msikilize hapa Jecha Salim Jecha akitoa taarifa yake kwa wanahabari:-