Alhamisi , 3rd Sep , 2020

Chuo kikuu cha Dar es salaam kimesema kuna uhitaji mkubwa wanafunzi kuchukua masomo ya ubunifu na ujasiriamali ili kuendana na soko la ajira ikiwa ni mikakati ya serikali katika kuinua soko la ajira na kufikia mapinduzi ya viwanda ikiwa na wasimamizi wabobevu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof Bernadetha Killian  jijini Dar es salaam wakati utiaji saini wa makubaliano ya miaka mitao na Generation empower ambao watawezesha vijana wanafunzi kusoma masomo hayo kwa ufadhili wao.

"Ni kweli kwa sasa uhitaji ni mkubwa kwakuwa mifumo imebadilika, uwezeshaji wa wanafunzi hawa utasaidia kupunguza utegemezi baada ya masomo yao ikiwemo kuhangaika na ajira" amesema Prof Kilian

Kwa upande wake mkurugenzi kitengo cha ubunifu na ujasiriamali Dkt Ambrose Itiika ameeleza kwamba soko la ajira kwa sasa linahitaji vijana kuwa wabunifu ma kuweza kujiajri badala ya kutegemea ajira toka serikalini."Nadhani kujiajiri kulingana na ubunifu ndio mkombozi kwa suala la ajira kwa vijana,kwahiyo ni vyema wakatumia nafasi hiyo ili kujifunza zaidi"