
Pichani Kuku aliyetolewa kwenye kizazi.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Simon Chacha, uchunguzi wa awali, tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina au ukatili kwa maana ya kuku huyo kuingizwa.
“Hakuwa na ujauzito alifika hospitali akadai anaumwa tumbo baada ya uchunguzi madaktari wakaona kifaranga cha Kuku kwenye kizazi na tayari wamekitoa, tukio hilo limefanyika nadhani kwa imani za kishirikina”, amesema Dkt. Simon.
Dkt. Ameongeza kuwa “Nimeagiza afanyiwe upasuaji ili kujihakikishia zaidi nini kimetokea ila kwa kufanyiwa kitendo hicho tayari ameharibiwa kizazi”.