Jumapili , 13th Sep , 2020

Tanzania hii leo inatarajia kupokea ugeni wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, atakayepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa ajili ya ziara ya ujirani mwema

Kushoto ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Taarifa hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali na katibu Mkuu anayetumikia Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Hassan Abbas

Aidha, mahusiano baina ya nchi hizi yamekuwa ni ya asili hii ni kutokana na ukaribu wa kijiografia na kihistoria baina ya nchi hizi, lakini pia utamaduni wa Uganda na Tanzania umekuwa ukishabihiana kutokana na muingiliano wa makabila ikiwemo kabila la wa Wahaya ambalo lipo Tanzania na baadhi ya maeneo ya Uganda

Lakini pia Tanzania na Uganda zimekuwa zikifungamana kisiasa pia, kwani zote kwa pamoja ni wanachama wa Jumuiya ya Nchi zinazounda Umoja wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataiafa (UN).