Jumatatu , 24th Oct , 2022

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kanda ya ziwa, imefanya ukaguzi wa vituo vya mafuta 121 na kubaini vituo 12 vinaendeshwa bila kuwa na bima hivyo kuhatarisha maisha ya wafanyakazi na wateja wao pindi yatakapotokea majanga ya moto.

Kituo cha mafuta

Meneja wa TIRA kanda ya ziwa Richard Toyota, amesema zoezi la ukaguzi wa vituo vya mafuta ni endelevu ili kuhakikisha vinakuwa na bima.

"Ni wastani wa asilimia kama 10 ya vituo vyote ambavyo havina bima na unaweza ukaona ni ndogo lakini kwenye majanga ni vituo vingi sababu unategemea endapo moto unatokea kwenye vituo vya mafuta unategemea nini, tunaandaa taarifa tunapeleka Ewura na wao watatusaidia kusimamia sheria yao, hivyo tunavitaka vituo vyote vya mafuta viwe na bima" amesema Meneja wa TIRA

Katika hatua nyingine Kaimu Meneja huyo amesema ipo mikakati ya wao kuongeza pato la Taifa kutoka asilimia 1.68 hadi asilimia 5 ikiwemo kutoa elimu ya bima kwa wananchi na kuunda kamati ya uhamamsishaji, "Kama nilivyotaka pale cha kwanza ni kuhakikisha tunapeleka elimu kwa wananchi kwa kufanya mihadhara mikutano Pamoja na vongozi mbalimbali wa kisiasa ili elimu iwafikie hatimaye tifikie lengo la ukusanyaji wa mapato tuliojiwekea".