Alhamisi , 30th Jul , 2015

Wananchi na wafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA Mkoa wa Njombe wamesema kuwa wanaimani na ujio wa Waziri mstaafu katika Umoja wao kwa kuongeza nguvu ya kuing'oa CCM madarakani.

Waziri Mkuu wa Zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akizungumza na Waandishi wa Habari hivi karibuni

Akizungumzia Ujio wa Lowassa katika umoja huo Diwani wa Chadema kata ya Njombe, Agrey Mtambo amesema kuwa Ukawa hauna nongwa nae na kuwa mtu akikiri hadharani kuachana na uovu haina shida.

Amesema kuwa ujio wake unakuja kuipa nguvu Chadema kupambana na CCM ambayo imekuwa ikiwaumiza kichwa kuiondoa madarakani.

Mtambo amesema kuwa anawakaribisha na watu wengine kujiunga na Ukawa ili wasaidie kuleta mabadiliko ya kuondoa chama kinacho wakandamiza Watanzania.

Amesema kuwa haina shida kuhamia chama hicho na ni faraja kwa kwa kuwa ujio wake unawaongezea hatua moja kuelekea Ikulu.