Alhamisi , 28th Jan , 2021

Waziri wa Maji Juma Aweso amewapa tahadhari wataalum wa Wizara ya Maji pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji kutokuchezea miradi ya maji kwani watashughulikia ipasavyo huku akisema wizara ya maji si wizara ya ukame.

Waziri wa Maji Juma Aweso

Akizungumza na wananchi wa Kahama mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, leo Januari 28, Aweso amesema  wizara yake itasiamma usiku na mchana kuhakikisha watanzania wanapata maji safi, salama na yenye kujitosheleza.

“Zipo kelele na malalamiko ambayo umetupa sisi wizara ya maji sisi tumeyapokea na tumeyasikia, nachotaka kuwaambia wataalamu wetu wa wizara ya maji na wakandarasi wanaotekeleza wizara ya maji vipo vya kuchezea ukishiba chezea kitambi au kidevu si miradi ya maji tutakushughulikia ipasavyo” amesema Aweso

Aidha Aweso amesema kuwa  wameweza kutekeleza miradi 48 ya maji  katika vijiji 69 huku miradi 24 bado ikiwa inaendelea na kuongeza kuwa  wamefanikiwa kuwakomboa akina mama wa Kahama kwa kutatua tatizo la maji.