Jumatano , 24th Aug , 2022

Taifa la Ukraine leo Agosti 24 limeadhimisha siku ya uhuru wake wa miaka 31 ikiwemo pia miezi 6 toka uvamizi wa Ukraine.  

Ulinzi mkali umeimarishwa kote nchi nzima kutokana na hofu ya kuwa Moscow inaweza kufanya mashambulizi mapya . 

Mikusanyiko ya shehere imezuiwa katika mji mkuu wa  Kyiv. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewaambia Waukraine katika hotuba ya kuadhimisha miaka 31 ya uhuru kuwa nchi yao ilizaliwa upya wakati Urusi ilipoivamia na kuwa haitasalimisha uhuru wake kwa ubabe wa Moscow. 

Zelensky amesema vita vitamalizika tu sio wakati mapigano yatasitishwa bali wakati Ukraine itakapoibuka mshindi. 

Rais huyo mwenye umri wa miaka 44 amesisitiza msimamo mgumu wa Ukraine ambao unapinga aina yoyote ya makubaliano ambayo yatairuhusu Moscow kudhibiti maeneo iliyoyakamata tangu kuanza kwa vita miezi sita iliyopita, yakiwemo maeneo ya kusini na mashariki mwa Ukraine.