Mwonekano wa Zanzibar Domino Commercial Tower
Jengo hilo la kibiashara litakapokamilika litaitwa Zanzibar Domino Commercial Tower, na litajengwa umbali wa kilometa 15 kutoka Mji Mkongwe katika eneo la hekta 20 ambapo pamoja na mambo mengine litakuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano utakaobeba watu 1,000 na Jengo la namna hiyo pia litakuwa la kwanza Afrika Mashariki na Kati.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa makubaliano baina ya kampuni ya Kitanzania ya AICL Group na kampuni ya XCassia yenye utaalamu na uzoefu wa kusanifu na kuchora ramani za majengo marefu duniani kupitia uongozi wa Edinburg Crowland Management Ltd yenye ofisi zake katika majiji ya New York na Dubai.