Jumapili , 15th Sep , 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Gutteres, ameziomba Serikali zote duniani kuheshimu utawala wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuruhusu mawazo ya watu na kuheshmu haki ya kila mmoja.

Antonio Gutteres, amesema hayo ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya demokrasiaduniani, ambapo amesema kila Taifa linatakiwa kujua demokrasia ni utawala unaowahusu watu.

Amesema kila Taifa linatakiwa kujua binadamu yeyote anatakiwa kuheshimiwa, kuthaminiwa, pamoja na kuhakikisha kwamba amani ya nchi inapatikana.

"Ikiwa leo ni Siku ya Demokrasia duniani, nazishauri nchi zote duniani kuheshimu haki ya kila mmoja, ushirikishwaji, pamoja na kusikilizana pia
niwashukuru wote ambao mnaopigania haya mpaka yanatokea katika mataifa yenu
" amesema Antonio Gutteres

September 15 ya kila mwaka, UN huadhimisha Siku ya Demokrasia duniani, ili kukumbushana mambo muhimu ya kuzingatia, katika kuhakikisha watu wanakuwa na uhuru wa mawazo.