Alhamisi , 24th Mar , 2016

Shirika la Umoja wa Kimatafaifa la Idadi ya Watu UNFPA limezindua teknolojia rahisi ya kutoa hudu

Shirika la Umoja wa Kimatafaifa la Idadi ya Watu UNFPA limezindua teknolojia rahisi ya kutoa huduma ya Mama na Mtoto kwa wakunga ili kuweza kuwajengea uwezo wakunga waweze kumhudumia vizuri mwanamke mjamzito kwa kutumia simu zao za mkononi..

Akiongea jijini Dar es salaam Afisa Mwandamizi wa kitengo cha mama na mtoto wa shirika la UNFPA Ferista Bwana amesema kuwa tekinologia hiyo itaweza kumkumbusha Mkunga jinsi ya kumhudumia mama mwenye uzazi pingamizi na matatizo mengine hivyo kumsaidia kiurahisi hata pale ambapo kunakuwa hamna mtaalam.

Mashine hiyo itakuwa msaada mkubwa hasa maeneo ya kijijini kwani maeneo hayo huwa na upungufu wa wataalam lakini mashine hizi hutoa mwongozop kwa wakunga jinsi ya kumuhudumia mama mjamzito na kurahisisha huduma kwa kinamama.

Kwa niaba ya serikali mkurugenzi wa mafunzo na maendeleao ya wataalam wa wizara ya afya Dkt Utilia Flavian Ngewere amesema kuwa wanaamini kinamama wengi zaidi watapata elimu ya kutosha kwani huduma zinazotolewa na kifaa hicho ni pamoja na jinsi ya kujiandaa kupata ujauzito, kutunza ujauzito, namna bora ya kujifungua, namna ya kumhudumia mtu aliekeketwa, lengo likiwa ni kupunguza hatari ya mwanamke kupoteza maisha wakati wa kujifungua.