
Imeripotiwa kuwa Rais wa Halmashauri kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ameitaka Ulaya kutafuta namna mpya ya kufadhili ulinzi wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi kwa kutumia fedha za Urusi zilizozuiwa barani Ulaya.
Baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kutuma jeshi lake nchini Ukraine mwaka 2022, Marekani pamoja na washirika wake zilizuwia mali za wafanyabiashara, benki kuu ya Urusi pamoja na za wizara ya fedha zipatazo dola bilioni 350.
Urusi imekosoa matumizi ya faida inayotokana na malipo ya riba kwa mali zake hizo ikiyaita kuwa ni wizi.