Ijumaa , 5th Jun , 2015

Makamanda wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ wameshauriwa kuweka mfumo bora utakaowezesha kushiriki katika mfuko wa kuweka na kukopa wa Ngome SACCOS kwa lengo la kuja kuwasaidia pale wanapostaafu.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Ngome SACCOS Kanali Charo Ateri wakati wa mkutano wa pamoja kati ya makamanda wa jeshi, wakuu wa vikosi, wakuu wa kamandi, na wanadhimu wa jeshi.

Kanali Ateri amesema kutokana na makamanda hao kuwa karibu na maafisa wa jeshi la askari wa jeshi hivyo itakuwa ni rahisi kwao kuwahamasisha na kuweza kujiunga na SACCOS hiyo.

Amesema kwa kuwaandalia wastaafu namna bora ya kuishi kutawasaidia kujikimu kimaisha tofauti na maisha ya awali jambo ambalo linawaweka wanajeshi watakaostaafu kutoshawishika na vitendo viovu.