Jumapili , 8th Mei , 2016

Mamaku wa Rais Samia Hassan Suluhu amewataka viongozi wa serikali katika maeneo mbalimbali nchini kuwajibika katika kuhakikisha wanasimamia vizuri bajeti ya serikali itakayopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Mama Samia ameyasema hayo Mkoani Dodoma wakati akifungua semina ya viongozi wa CCM ambapo amewakumbusha wajibu wao katika utendaji wa kuwahudumia wananchi.

''Utumbuaji majipu hautaishia tuu kwa viongozi wa juu utashuka chini pia kwa watendaji hasa ambao hawatasimamia shughuli mbalimbali katika maeneo yao na kusababisha kutokea kwa ubadhirifu wowote nao watatumbuliwa''- Amesema Mama Samia

Kwa upande wake Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema inabidi kutizama namna ya kutunga sheria ndogo ambayo itawezesha madiwani kuweza kuwawajibisha watu walio chini yao ili kuongeza ufanisi wa utendaji.