Ijumaa , 1st Apr , 2016

Wananchi wa Kata ya Enduimet iliyoko Mji mdogo wa Mirerani Mkoani Manyara, wamelalamikia viongozi wa serikali za mitaa na vitongoji kwa uhusika na uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya wananchi jambo linalozua mgogoro.

Bi. Joyce Mziray mmoja wa Waathirika wa Uuzaji wa ardhi wa eneo la Enduimet, Mererani, Manyara.

Wakizungumza na East Africa Radio, wananchi hao ambao ni wahanga wa mgogoro huo wa ardhi ambao wanakiri kuwa waliuziwa eneo lililopo pembezoni mwa eneo la EPZ lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa madini ya Tanzanite hivyo kutakiwa kuondoka katika eneo hilo licha ya kumiliki maeneo hayo kihalali huku wakiwa hati zilizosainiwa na viongozi wa serikali.

Mgogoro huo umechukua sura mpya hasa pale ilipobainika kuwa eneo la EPZ linalohusishwa halijapimwa na halina mipaka rasmi inayotenganisha eneo hilo na maeneo ya wananchi pia kukosekana kwa mipaka kati ya vijiji na vijiji hivyo kupelekea mgongano baina ya wananchi na viongozi wao

Diwani wa Kata ya Enduimet, Philemon Oyogo, amesema kuwa viongozi wa serikali na wataalamu wasiokuwa na maadili ambao waliwauzia wananchi maeneo ya EPZ na kuwapatia hati halali za kumiliki maeneo hayoa ambayo waliyaendeleza na kuwajenga jambo amabalo linaweza kuleta hasara hivyo amemtaka mkuu wa wilaya ya Simanjiro awawaji bishe viwanda.

Mkuu wa Wilaya ya Simajiro Mahamoud Kambako ambaye alikua akisubiriwa na wananchi ambao hawakuchoka kusubiri na hata kunyeshewa na mvua huku wakisubiri majibu ya serikali ambako ameahidi kuunda tume ya kushughulikia tatizo hilo na kuipa muda wa siku 4.

Karibu asilimia 70% ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani ni wa pangaji hivyo hitaji la ardhi ya makazi ni kubwa hivyo mamlaka zinapaswa kupima maeneo kwa ajili ya makazi na kuwagawia wananchi ardhi.

Sauti ya Joyce Mziray na Kanaeli Minja wakizungumzia madhila yaliyowakuta