Ijumaa , 26th Nov , 2021

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, ameusifia mradi wa kuendeleza ufukwe wa Coco, baada ya kutengenezwa vibanda vya kisasa katika eneo ambalo hufanyika biashara ya mihogo.

Kushoto ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, na kulia ni mwonekano mpya wa Coco Beach

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto Kabwe, ameshauri kwamba katika kuendelea kuviboresha zaidi ni vyema ikawekwa nishati ya umeme wa jua.

"Hivi vibanda hapa Coco Beach vinapendeza, nataraji kuwa wahusika wamefikiria vema suala la nishati, ingependeza sana kama kungewekwa solar panels juu ya vibanda vyote, any company to consider CSR there?", ameandika Zitto Kabwe