Jumatano , 23rd Aug , 2017

Mtoto Frank Jewa mwenye umri wa miaka 15 mkazi wa Mwanza, ametelekezwa na shangazi yake aliyetambulishwa kwa jina la Rebeca, akiwa anatokea Mwanza kuja jijini Dar es Salaam ambako shangazi yake huyo anaishi.

Mtoto Frank Jewa akiwa na mdogo wake

Frank ambaye yupo na mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 9 mwenye ulemavu, amesema alitoka Mwanza kwa mama yake mlezi kuja Dar es salaam kwa shangazi yao, ambaye aliambiwa amewaita kwa mujibu wa mama yake mlezi aliyemsafirisha.

Frank anasema alipofika Dar es salaam shangazi yake huyo hakupatikana kwenye simu, na kumpa hisia kuwa huenda shangazi yao huyo hakutaka waende nyumbani kwake, kutokana na hali zao.

Akiendelea kuelezea tukio hilo Frank anasema mama yake mzazi alikimbia nyumbani kwao akiwa na mtoto mwengine mdogo, kwa sababu baba yao alitaka kumchoma kisu kutokana na ugomvi ambao ulitokea.

Tazama video ya mtoto huyo akielezea tukio zima mpaka kufika Dar es salaam na jinsi alivyotelekezwa.