
Hii ni baada ya mtoto wa miaka minane kuripotiwa kuuawa na mbwa huyo ajulikanae kwa jina maarufu la bull dog, tukio lililotokea Jumamosi iliyopita .
Afrika Kusini ina moja ya matukio makubwa ya vifo vinavyohusiana na mashambulizi ya mbwa duniani ikilinganishwa na idadi ya watu wake, kulingana na ripoti.
Mwezi Oktoba, mvulana wa miaka 10 aliuawa na bull dog wawili wanaomilikiwa na familia moja.
Zaidi ya watu 50,000 wametia saini ombi la mtandaoni la kupiga marufuku mbwa hao kama wanyama wa nyumbani nchini Afrika Kusini.