Ijumaa , 29th Apr , 2016

Zaidi ya Vijana 1000 wanaotoka katika mazingira hatarishi kutoka wilaya za Ilala na Temeke Jijini Dar es Salaam,wamenufaika na mradi wa soko la ajira ambao umewasaidia kupata stadi za maisha na kupata ajira katika taasisi mbalimbali nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika chuo cha Future Word, kilichopo jijini Dar es Salaam,vijana hao wamesema mradi huo umewasaidia kutoka katika utegemezi kutoka katika familia zao na kuwawezesha kujiari wenyewe.

Vijana hao wanajifunza ufundi wa aina mbalimbali, ikiwemo mafunzo ya uhudumu wa hoteli pamoja na usajiriamali wa aina tofautitofauti katika kukabiliana na tatizo hilo la ajira.

Kwa upande wake Meneja wa shirika la kuwazesha vijana kiuchumi kutoka shirika la Plan, Simon Ndembeke amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuunga mkono serikali la kutatua tatizo la ajira kwa vijana nchini.

Nae Mkuu wa Chuo hicho Robert Mkola amesema chuo hicho kinafanya tathimi ili kuwapa vijana mafunzo yanayowasaidia kupata ajira katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi.