
Mchungaji Philipo Mafuja
Wito hao umetolewa mkoani Mwanza katika ibada ya Kitaifa iliyoongozwa na Mchungaji Philipo Mafuja ambaye alizungumzia umuhimu wa viongozi nchini kuzingatia misingi ya dini ndani ya jamii.
Akizungumza kwenye ibada ya Krismasi kitaifa iliyofanyika katika Kanisa la AICT Makongoro mkoani Mwanza ambapo ibada hiyo ilianza kwa maombi yaliyongozwa na Mchungaji Philipo Mafuja ambaye alizungumzia umuhimu wa kuzingatia utawala wa sheria.
Mchungaji Mafuja ameongeza kuwa kama viongozi wakizingatia utawala wa haki ni wazi Tanzania itakua nchi ya kipato cha kati kwa kuwa na viwanda vingi na kufanikisha kuondoa umaskini kwa nchi na kwa mtu mmoja mmoja.
Waumini wa dini ya Kikristo nchini Tanzania leo wameungana na wenzao duniani katika kusherehekea kuzaliwa kwa mwokozi wao Yesu Kristo, ambapo ujumbe wa amani, upendo na kuzingatia utawala wa haki umetolewa