Jumatano , 27th Jul , 2022

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewataka viongozi kufanya kazi ya kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao badala ya kuwaongoza kwa kuwawekea sheria na miongozo ya kuwarudisha nyuma.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana

Makamu Mwenyekiti Kinana amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, haitaki kumuacha mwananchi yeyote nyuma kwa vikwazo visivyo na tija ikiwemo Kodi zisizo na afya kwa uanzishwaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo biashara.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amewakumbusha wananchi kuhusu sensa ya watu na makazi na kuwasihi kujitokeza kwa wingi ili kuiwezesha serikali kupanga mipango yake ya maendeleo.