Jumatano , 19th Aug , 2015

Vyombo vya habari vimekumbushwa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kufuata misingi ya maadili ya sekta hiyo ili kupata viongozi bora katika uchaguzi wa mwaka huu.

Chiku Abwao akiongeana wananchi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wahadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa.

Mgombea wa ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia‭ ‬chama cha ACT-Wazalendo‭ ‬Mhe.‭ ‬Chiku Abwao amewashauri wanahabari kujiepusha na rushwa ili kutekeleza majukumu yao kwa haki.

Aidha,‭ ‬amesema ameamua kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo ili kuleta mageuzi thabiti ya kujenga nchi.

Hata hivyo,‭ ‬Mhe.‭ ‬Chiku Abwao amewakumbusha wananchi kutambua viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu badala ya kutanguliza ushabiki wa vyama vya siasa.