Jaji Mkuu wa Kenya david Maraga
Mwanasheria Adrian Kamotho Njenga ambaye ndiye aliyeandika barua hiyo, ameifikisha mbele ya bunge la Kenya akimtuhumu Jaji Mkuu David Maraga na wengine 6, kukiuka katiba ya nchi hiyo na matumizi mabaya ya mamlaka.
Mr. Kamotho amesema Majaji hao wakiwemo Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Jaji Mohamed Warsame, Jaji Aggrey Muchelule, Prof . Tom Ojienda, Bi. Emily Ominde na Mercy Deche hawastahili kushika wadhifa huo.
“Makamishna wa Mahakama waliotajwa hapo awali wameshindwa kukuza na kuwezesha uhuru na uwajibikaji wa Mahakama na uwazi wa mahakama, kinyume na Ibara ya 172 (1) ya Katiba”, amesema Mr. Kamotho.
Barua hiyo ambayo imepokelewa na Tume ya Utumishi ya Bunge Jumatatu ya tarehe 26, imesema watumishi hao wa juu wa serikali wamevunja sura ya 6 ya katiba kuhusu uaminifu.
Ikumbukwe kwamba Jaji david Maraga ndiye aliyetengua matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8, 2017, ambayo yalimpa ushindi Uhuru Kenyatta, na Muunganiko wa vyama vya upinzani nchini kenya (NASA) kufungua kesi, ambayo matokeo yake ndio yalikuwa kufutwa kwa uchaguzi huo na kutaka kurudiwa upya.




