Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Augustine Lyatonga Mrema amesema kususia vikao vya Bunge kunawanyima fursa wananchi haki ya kuwasilishiwa mawazo yao juu ya maendeleo ya nchi hivyo ni lazima taratibu za Bunge zifuatwe.
''Kama wanataka Tulia Ackson aondoke kuna kanuni za kufanya hivyo kwani watazira hadi lini na yule mama ameendelea kukalia kile kiti, wabunge wa upinzani waytafakari upya msimamo wao''-Amesema Mrema.
Kwa upande Mwingine Mhe. Mrema amesema hafurahishwi na mwenendo wa vyama vya upinzani, na hata sita kuzungumzia namna vyama hivyo vinavyofanya siasa za chuki na kutowajali wananchi waliowachagua.
''Mimi ni mpinzani mzalendo na mkweli nitawasem wapinzani na hata viongozi wa CCM ambao hawafuati katiba, haki za binadamu pamoja na mafisadi ambao wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi''- Amesema Mrema.





