Jumatano , 13th Feb , 2019

Msanii Godzilla ambaye amefariki dunia alfajiri ya leo, alizungumza juu ya kifo chake siku chache zilizopita, kwenye mtandao wa twitter ambao alikuwa akipenda sana kuutumia.

Kwenye ukurasa wake mnamo februari 9, Godzila aliandika ujumbe kuwa hata kama akifa, jina lake litaendelea kubaki kwa watu, jambo ambalo limetafsiriwa kama alikuwa anakaribia kufikwa na umauti.
 

Hata hivyo Godzilla aliendelea kutumia ukurasa huo mpaka jana saa 9 alasiri, ambapo alitweet ujumbe wake wa mwisho, ambao ulisomeka hivi.

 

Kutokana na kifo cha Godzilla Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa ujumbe uliolezea kusikitishwa kwake  na msiba huo, huku akisema kwamba Godzilla alikuwa na ndoto nyingi ambazo zimezimika ghafla