Jumatatu , 3rd Aug , 2015

Watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam wametakiwa kuongeza kasi ya utumiaji wa mifumo ya kilektroniki kulipia huduma zinazotlewa katika mamlaka hiyo ili kuongerza ufanisi wa kazi na kuondoa ucheleweshaji wa uondoaji wa Mizigo.

Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam (kushoto), Bw.Hebel Mhanga akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na wadau

Akiongea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika mkutano na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari TPA, Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam bw, Hebel Mhanga amesema matumizi sahihi ya njia za kilektroniki yatasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza ufanisi katika bandari.

Bw, Mhanga amesema wakati sasa umefika kwa wadau wa bandari kuzoea matumizi ya kielektroniki hasa katika malipo ili kupunguza ubadhirifu pamoja na mianyta ya rushwa.

Alifafanua kuwa kwa sasa hakuna sababu ya mteja kwenda bandarini kufanya malipo bali mifumo hiyo hiyo inawezesha kulipia mahali mteja alipo na kwenda moja kwa moja eneo la kutolewa mzigo.