Jumanne , 31st Mei , 2016

Wafanyabiashara wa Samaki wabichi Mkoani Mbeya wameilalamikia serikali ya mkoa huo kutangaza kuwa samaki wabichi wanaouzwa kwenye maduka yaliyopo Jijini humo kuwa wana sumu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.

Wakiongea na waandishi wa Habari Jijini humo Umoja wa Wafanyabiashara hao wamesema kuwa hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kusema samaki wengi wanaogaziwa kutoka china wanasumu wamefanya biashara yao kudorora.

Wamesema kufuatia tamko hilo wateja wengi wa samaki wameacha kununua kitoweo hicho kwani hawajui ni aina gani ya samaki wanaotajwa kuwa na madhara kwa binadamu.

Hivi karibuni Makalla alitoa tamko na kusema kwamna samaki wabichi wanaopitia katika mipaka ya mkoa huo wakitokea nchini China wana kemikali zinazosababisha wanawake kuota ndevu na wanaume kuota matiti.