Jumamosi , 22nd Oct , 2022

Serikali Wilaya ya Morogoro imesema haitakubaliana na hatua ya wafugaji ambao wanaingiza mifugo yao kwenye vyanzo vya maji ambavyo vinatiririsha maji kwenye mto Ruvu unategemewa na wakazi zaidi ya milioni saba wa mikoa ya Morogoro, Pwani pamoja na Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando

Hatua hiyo imekuja ili kunusuru kuttokea kwa uhaba wa maji kwenye mikoa hiyo kutokana na kuwepo kwa ukame wa muda mrefu ambao umepelekea mito mingi ambayo inapeleka maji kwenye mto Ruvu kupungua, huku chanzo kingine kikitajwa kuwa ni wafugaji kuingiza mifugo kwenye vyanzo vya maji kutafuta malisho pamoja na maji kwa ajili ya mifugo.

Akizungumza na Wafugaji wa Wilaya ya Morogoro Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando anaeleza msimamo wa Wilaya hiyo kuhusu utunzanji wa vyanzo vya maji huku Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy akieleza hali waliyokutana nayo baada ya kuanza kukagua mito hiyo.