
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo alipofanya ziara katika Shamba la Mifugo la Maloloi lililopo Kijiji cha Milama Kata ya Dakawa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ili kujionea namna mtanzania huyo mwenye asili ya kimasai alivyobadilisha ufugaji wa kiasili na kufuga kisasa, kwa kuwa na mifugo bora, maeneo ya kuhifadhia mifugo pamoja na kujenga nyumba za kisasa.
Amesema wafugaji wanatakiwa kubadilika na kuondokana na migogoro ya ardhi pamoja na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa hivyo ni muhimu kwao kuacha ufugaji wa kuhamahama badala yake wanunue ardhi na kuimiliki kisheria na kufuga mifugo ambayo wana uwezo wa kuihudumia.
“Ni muhimu sana wanunue ardhi na waimiliki kwa mujibu wa sheria, inasajiliwa kwa ajili ya ufugaji anaweka na miundombinu kama majosho na kisima kikubwa cha maji kwa ajili ya uhakika wa kupata maji muda wote, itasaidia sana kufanya sekta inakuwa na mchango mkubwa.” Amesema Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Aidha, amewataka wataalam wa sekta ya mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kufika katika shamba la mifugo la Maloloi kumsadia mmiliki wa shamba hilo kulisajili pamoja na kulitambua kuwa ranchi ya sekta binafsi kwa wafugaji wa asili waliobadilika.