Ijumaa , 6th Mei , 2016

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa Tanzania nzima kwa mwaka kunakuwa na wagonjwa elfu 38 wa saratani na wagonjwa elfu 35 wanafariki dunia.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Julius Mwaiselage

Dkt. Mwaiselage ametoa takwimu hizo leo jijini Dar es Salaam kwenye mahojiano maalumu na East Africa Television na kuongeza kuwa wagonjwa wengi wanaofika hospitalini hapo kupatiwa matibabu wanakuwa tayari wamefika katika hatua mbaya ya ugonjwa na kupelekea wagonjwa hao kuhitaji kutumia matibabu ya gharama kubwa na wengi wao wanashindwa kulipia baadhi ya huduma kama zile za dawa.

Kwa upande wake mtaalamu wa magonjwa ya Saratani nchini Dkt. Crispin Kahesa, amesema mikoa inayoongoza kwa saratani nchini ni mikoa yenye idadi kubwa ya watu ya Dar es Salaam, Mwanza pamoja na Mbeya.